Bi Zuleikha Juma Hassan alisema barabara ya Dongo Kundu ni kiungo kinachorahisisha usafiri katika kipindi ambacho barabara ya Kinango–Kwale bado haijakamilika.
Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir, alipokagua mradi huu wiki iliyopita, alisema reli iko tayari na inatarajiwa kuhudumia abiria wapatao 4,000 kwa siku.