AVDelta News
Skip to main content Skip to page footer

Usiyoyajua kuhusu Mlango wa Bahari wa Hormuz

Rais wa Marekani Donald Trump amewataka washirika wa NATO kutoka nchi saba wamsaidie kuulinda Mlango wa Bahari wa Hormuz wakati Iran imeonya meli za ‘maadui’ dhidi ya kuonekana hapo.

Tangu mgogoro kati ya Marekani, Israeli na Iran ulipozidi Februari 2026, kila mtu ameanza kuangalia kwa makini habari kuhusu Mlango wa Bahari wa Hormuz.

Awali ulionekana kama mstari tu kwenye ramani, lakini sasa umegeuka kuwa kitovu cha kijiografia na kisiasa kinachoweza kubadilisha bei za mafuta na kuchelewesha usafirishaji wa bidhaa muhimu duniani.

Mlango huo wa Bahari wa Hormuz unaunda daraja muhimu kati ya Ghuba la Ajemi na Bahari ya Arabia, sehemu ya Bahari Hindi.

Nafasi yake nyembamba zaidi ni kilomita 34 pekee, kati ya pwani ya Iran upande wa kaskazini na Musandam Peninsula ya Oman upande wa kusini.

Hapa ndipo yanapopita karibu asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa baharini duniani.

Hali tete ya kisiasa au mabadiliko mzozo wowote vinaweza kuathiri usafirishaji wa meli na kusababisha ucheleweshaji wa mizigo.

Tahadhari kwa meli zinazopita

Kwa kuwa mkono huu wa bahari ni mwembamba sana na meli nyingi hupita kila siku, wale wanaosafirishia mizigo wanapaswa kuwa makini kila wakati.

Hali yoyote isiyo thabiti, iwe ni mgogoro wa kisiasa au shughuli za kijiografia, inaweza kufanya meli kusogea polepole, kuchelewa kufika, au kubadilisha njia, jambo linaloathiri bei za bidhaa na mafuta duniani.

Athari kwa uchumi wa dunia

Sehemu ndogo kama hii, ndogo kwa ukubwa lakini kubwa kwa athari, ina maana kubwa kwa uchumi wa dunia. Hali yoyote inayotokea hapa inaweza kupandisha bei za mafuta kutoka Nairobi hadi New York, kuchelewesha mizigo muhimu, na kuathiri biashara na soko la fedha duniani.

Kwa hivyo, Mlango wa Bahari wa Hormuz ni kitovu cha dunia kinachotazamwa kwa makini na kila mtu.